Shule ya Msingi Sanjo yaneemeka, yapokea Shilingi Milioni 6.6 kupitia Harambee
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mhe. Erasto Machibya atoa pongezi za dhati kwa upatikanaji wa Shilingi Milioni 6,630,200/= kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Shule ya Msingi Sanjo iliyopo kata ya Usagara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Akitoa pongezi hizo leo Tarehe 31 Mei 2025 katika Harambe ya Ujenzi na ukarabati wa Shule ya Msingi Sanjo na kutoa shukrani za dhati kwa Mdau wa Maendeleo Bw. Photunatus Kafumu kwa kuwa mchangiaji na kufanikisha sehemu ya upatikanaji huo wa fedha na kutoka kwa Wadau wa Maendeleao pamoja na Wananchi ambapo Mchango huo utakua Mwarobaini kutatua changamoto iliyokuepo ya Wanafunzi wa shule hio kukaa katika Mazingira ambayo sio rafiki kimasomo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi Bw. Crispine Shami amesema kuwa ni hatua ku wa sana kufanya na shule hiyo na ikawe shule ya kuigwa ambapo kwa hatua hiyo ameahidi pia kufikisha maombi ya Kiasi cha Milioni mbili kutoka Halmashauri ziweze kugawanywa ambapo Milioni moja itafika Shule ya Msingi Sanjo ili kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma katika Mazingira salama.
Naye Mwalimu Mwenyekiti wa kijiji cha sanjo Bw. Bahati Msoke ashukuru kwa kupokea kiasi cha fedha cha Shilingi Milioni 6,630,200/= ambapo kiasi cha shilingi Milioni 5,980,000/= ni fedha taslimu zilizopatikaba na shilingi 6,5000/= ikiwa ni ahadi vilevile michango mingine ni pamoja na simenti mifuko 46 ,mchanga tripu 5 na matofari 3200
No comments:
Post a Comment